TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 98)

 1. 1. Mwimbie Mungu, wimbo mpya kwa furaha;

  Tangaza matendo yote afanyayo.

  Msifu yeye, Ndiye Mungu wa ushindi;

  Anapohukumu,

  hutenda kwa haki.

  (KORASI)

  Imbeni!

  Twimbe wimbo mpya.

  Imbeni!

  Yehova Mfalme.

 2. 2. Shangilieni, pigeni vigelegele;

  Jina lake sifu, na kumtukuza.

  Jiunge nasi, tumwimbie Bwana wetu,

  Piga tarumbeta,

  kinubi na zeze.

  (KORASI)

  Imbeni!

  Twimbe wimbo mpya.

  Imbeni!

  Yehova Mfalme.

 3. 3. Bahari navyo vilivyomo vimsifu,

  Uumbaji wote umwimbie sifa.

  Mito, vijito, vyote vipige makofi,

  Milima, vilima,

  vimsifu Yeye.

  (KORASI)

  Imbeni!

  Twimbe wimbo mpya.

  Imbeni!

  Yehova Mfalme.