TAZAMA
Maandishi
Picha

(Methali 3:1, 2)

 1. 1. Njia ya kweli, ni njia bora sana,

  Uamuzi ni wako wewe.

  Na mashauri ya Yehova utii;

  Umtumaini Yeye.

  (KORASI)

  Shika ukweli.

  Kwako uwe halisi.

  Utapata shangwe

  ya Yehova

  Ukishika ukweli.

 2. 2. Bidii yako, na jitihada zako,

  Katika kazi ya Ufalme,

  Zitatokeza baraka za milele,

  Na tumaini jangavu.

  (KORASI)

  Shika ukweli.

  Kwako uwe halisi.

  Utapata shangwe

  ya Yehova

  Ukishika ukweli.

 3. 3. Kama watoto, twahitaji mwongozo,

  Mashauri na mwelekezo.

  Na tutembee kila siku na Mungu;

  Tupate baraka zake.

  (KORASI)

  Shika ukweli.

  Kwako uwe halisi.

  Utapata shangwe

  ya Yehova

  Ukishika ukweli.