TAZAMA
Maandishi
Picha

(Mathayo 10:28)

 1. 1. Watu wangu msisite,

  Ufalme tangazeni.

  Msihofu adui.

  Wote hubirieni.

  Mwana wangu, Kristo Yesu,

  Katimua Shetani,

  Atamfunga karibuni,

  Kisha kuwe amani.

  (KORASI)

  Watu wangu msihofu.

  Nitawapa wokovu.

  Nitalinda wa’minifu,

  Kama mboni ya jicho.

 2. 2. Japo adui ni wengi,

  Japo wanawatisha,

  Japo wanawacheka,

  Ili kuwapotosha,

  Msihofu watu wangu;

  Pigeni moyo konde.

  Nitatunza wa’minifu,

  Hadi Har–Magedoni.

  (KORASI)

  Watu wangu msihofu.

  Nitawapa wokovu.

  Nitalinda wa’minifu,

  Kama mboni ya jicho.

 3.  3. Sitawasahau kamwe;

  Nitawapa ulinzi.

  Hata mfe shambani,

  Kifo kitanitii.

  Hata wakiua mwili;

  Nafsi hawataweza.

  Iweni waaminifu,

  Nami nitawakweza.

  (KORASI)

  Watu wangu msihofu.

  Nitawapa wokovu.

  Nitalinda wa’minifu,

  Kama mboni ya jicho.