TAZAMA
Maandishi
Picha

(Mathayo 22:37)

 1. 1. Nakupa moyo wangu,

  Nipende kweli yako.

  Ninakupa sauti,

  Ikuimbie Bwana.

 2. 2. Ninakupa miguu,

  Mikono yangu pia.

  Nakupa mali zangu,

  Zifanye kazi yako.

 3. 3. Ninakupa uhai,

  Nifanye upendayo.

  Nichukue nifanye,

  Mapenzi yako Bwana.