TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 139)

 1. 1. Mungu, wanijua vizuri,

  Nilalapo na niamkapo.

  Na fikira zangu umechunguza,

  Maneno na matendo yangu

  wajua.

  Sirini nilipofanyizwa,

  Uliiona mifupa yangu.

  Yote yalikuwa yameandikwa.

  Unastahili sifa

  na utukufu.

  Ee, Yehova, una hekima nyingi;

  Nafsi yangu inajua vema.

  Hata katika giza la usiku,

  Roho yako itaniongoza.

  Yehova nijifiche wapi,

  Kutoka mbele za uso wako?

  Si Kaburini wala si mbinguni,

  Gizani wala baharini,

  siwezi.