TAZAMA

(Zaburi 4:1)

 1. 1. Yehova nakuomba:

  ‘Sala yangu sikia.’

  Vidonda vyangu haviponi;

  ninalemewa.

  Nimevunjika moyo

  na kukata tamaa.

  Yehova Mungu wa faraja,

  ninakusihi.

  (KORASI)

  Niinue; nipe nguvu.

  Nifariji, Niongoze.

  Naja kwako. Ee Yehova,

  Mungu wangu, Nguvu zangu.

 2. 2. Neno lako lanifariji,

  lanipa nguvu.

  Lafunua hisia zangu

  za ndani sana.

  Niwezeshe kulitumaini

  Neno lako.

  Wewe U mkuu kuliko

  mioyo yetu.

  (KORASI)

  Niinue; nipe nguvu.

  Nifariji, Niongoze.

  Naja kwako. Ee Yehova,

  Mungu wangu, Nguvu zangu.