TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 95:2)

 1. 1. Yehova Mungu tunakushukuru,

  Twaja kwako kupitia sala,

  Nasi tunainama mbele zako,

  Twajiweka mikononi mwako.

  Sisi ni watenda dhambi, wanyonge;

  Tunakuomba utusamehe.

  Kwa damu ya Mwanao tusafishe,

  Wajua umbo letu vizuri.

 2. 2. Twakushukuru kwa fadhili zako,

  Asante kwa kutuvuta kwako.

  Utufundishe kukujua wewe,

  Twataka tuwe waaminifu.

  Una nguvu zisizo na kifani,

  Asante kwa kutujasirisha.

  Tusonge mbele kwa unyenyekevu;

  Ee Yehova wastahili sifa!