TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 23)

 1. 1. Yah ni Mchungaji wangu;

  Namfuata yeye.

  Anaujua moyo wangu,

  Sitakosa chochote.

  Penye maji hunileta,

  Ananiburudisha.

  Upendo wake huniongoza

  Nipate pumziko.

  Upendo unaniongoza,

  Nipate pumziko.

 2. 2. Njia zako zapendeza,

  Njia zako za haki.

  Usiniache nipotee;

  Nisije kukuacha.

  Nijapopita bondeni;

  fimbo yaniongoza.

  Sitaogopa lolote kamwe,

  Ninakutegemea.

  Siogopi lolote kamwe,

  Ninakutegemea.

 3.  3. Ndiwe mchungaji wangu!

  Nakufuata wewe.

  Wanitegemeza daima,

  Mahitaji wanipa.

  Wategemeka hakika,

  Kama unavyoishi.

  Na fadhili zako za upendo,

  Zinifuatilie.

  Fadhili zako za upendo,

  Zinifuatilie.

(Ona pia Zab. 28:9; 80:1.)