TAZAMA
Maandishi
Picha

(1 Petro 5:10)

 1. 1. Kweli yake Mungu amekufundisha,

  Amekutoa katika giza.

  Aliona moyo wako watamani,

  Kufanya mambo yaliyo mema.

  Kwa sala ulijiweka wakfu;

  Daima atakuimarisha.

  (KORASI)

  Kwa damu ya Mwanaye,

  alikununua.

  Hukuimarisha,

  na kukupa nguvu.

  Atakulinda na

  kukuongoza wewe.

  Hukuimarisha,

  na kukupa nguvu.

 2. 2. Katoa Mwanaye, kwa niaba yako;

  Hivyo, ataka ufanikiwe.

  Basi kama Mungu alifanya hivyo,

  Bila shaka atakupa nguvu.

  Imani yako hatasahau;

  Walio wake atawatunza.

  (KORASI)

  Kwa damu ya Mwanaye,

  alikununua.

  Hukuimarisha,

  na kukupa nguvu.

  Atakulinda na

  kukuongoza wewe.

  Hukuimarisha,

  na kukupa nguvu.