TAZAMA
Maandishi
Picha

(Wafilipi 1:10)

 1. 1. Twahitaji utambuzi,

  Kujua mambo yafaayo,

  Ambayo ni muhimu zaidi

  Tupasayo kufanya!

  (KORASI)

  Penda mema; Mungu wetu

  Afurahi.

  Tuchukie mabaya. Tusali

  Na kufanya

  Yaliyo muhimu zaidi.

 2. 2. Nini kingine chenye maana

  Kuliko kuhubiri?

  Na kutafuta kondoo wa

  Mungu waliopotea?

  (KORASI)

  Penda mema; Mungu wetu

  Afurahi.

  Tuchukie mabaya. Tusali

  Na kufanya

  Yaliyo muhimu zaidi.

 3. 3. Tukifanya yaliyo muhimu,

  Tutapata uradhi.

  Na amani ya akili

  Ipitayo zote tupate.

  (KORASI)

  Penda mema; Mungu wetu

  Afurahi.

  Tuchukie mabaya. Tusali

  Na kufanya

  Yaliyo muhimu zaidi.