TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 55)

 1. 1. Ee Yehova nakuomba,

  Usijifiche mbali.

  Sikiliza, unijibu,

  Ili nisiogope.

  (KORASI)

  Mtupie Yah mzigo;

  Naye atakutegemeza.

  Hataacha utikiswe,

  Atakuimarisha.

 2. 2. Kama ningekuwa njiwa,

  Ningeruka nyikani,

  Mbali na watu waovu,

  Watendao jeuri.

  (KORASI)

  Mtupie Yah mzigo;

  Naye atakutegemeza.

  Hataacha utikiswe,

  Atakuimarisha.

 3. 3. Yehova hutufariji,

  Na kutupa amani.

  Ijapo tunalemewa,

  Ana fadhili nyingi.

  (KORASI)

  Mtupie Yah mzigo;

  Naye atakutegemeza.

  Hataacha utikiswe,

  Atakuimarisha.