TAZAMA
Maandishi
Picha

(Mathayo 26:26-30)

 1. 1. Yehova uliye mbinguni,

  Ni usiku wa pekee!

  Usiku huu kale, ulionyesha,

  Upendo, haki, hekima.

  Mwana-Kondoo wa Pasaka,

  Kawalinda watu wako.

  Karne nyingi baadaye Kristo Yesu,

  Akatoa uhai wake.

 2. 2. Mkate huu na divai,

  Vinatukumbusha mengi.

  Ulitoa zawadi ya Mwana wako,

  Ilikugharimu sana.

  Twafanya Ukumbusho huu;

  Kumkumbuka Mwanao;

  Jinsi kifo chake kilivyoandaa,

  Ukombozi kutoka kifo.

 3.  3. Mbele zako tumekutana,

  Umetualika kwako.

  Twakusifu wewe kwa upendo wako,

  Twaheshimu jina lako.

  Ukumbusho wakutukuza,

  Watuchochea moyoni.

  Tufuate hatua za Kristo Yesu,

  Kisha uzima wa milele.