TAZAMA
Maandishi
Picha

(Sefania 2:3)

 1. 1. Mataifa yote,

  Yanampinga Kristo.

  Muda wao umekwisha.

  Mungu ameagiza.

  Siku zao kwisha;

  Ufalme utadumu.

  Kristo ataponda adui.

  Hatakawia kamwe.

  (KORASI)

  Mtafuteni Yehova,

  Mtegemeeni Yeye.

  Utafuteni,

  Uadilifu.

  Tegemeza enzi yake.

  Mungu atakukomboa,

  Kwa nguvu zake.

 2.  2. Twapa wote fursa,

  Ya kusikia Neno.

  Waamue wapendavyo,

  Uchaguzi ni wao.

  Japo majaribu,

  Hatuogopi kamwe.

  Mungu husikia maombi,

  Ya watumishi wake.

  (KORASI)

  Mtafuteni Yehova,

  Mtegemeeni Yeye.

  Utafuteni,

  Uadilifu.

  Tegemeza enzi yake.

  Mungu atakukomboa,

  Kwa nguvu zake.