TAZAMA
Maandishi
Picha

(Waebrania 1:6)

 1. 1. Tumsifu Mwana,

  Wa kwanza wa Yehova.

  Mfalme mteule,

  Baraka ataleta.

  Atawala kwa haki,

  Fahari, heshima.

  Naye atatetea,

  Enzi ya Yehova.

  (KORASI)

  Tumsifu Mwana,

  Wa kwanza wa Yehova!

  Kristo ametawazwa,

  Naye anatawala!

 2. 2. Tumsifu Mwana,

  Wa kwanza wa Yehova.

  Alilipa fidia;

  Tupate msamaha.

  Bibi-harusi wake,

  Ametayarishwa.

  Utawala wa Mungu,

  Ushike hatamu.

  (KORASI)

  Tumsifu Mwana,

  Wa kwanza wa Yehova!

  Kristo ametawazwa,

  Naye anatawala!