TAZAMA
Maandishi
Picha

(Kutoka 15:1)

 1. 1. Mwimbieni Yah! Anastahili kusifiwa.

  Majeshi ya Wamisri, kafa baharini.

  Msifuni Yah;

  Mungu asiye na kifani.

  Yeye ni Yehova,

  Amepata ushindi.

  (KORASI)

  Yah Yehova, Uliye juu,

  Yuleyule wa tangu milele,

  Utaharibu adui zako,

  Jina lako litakaswe.

 2. 2. Wote ambao wanashindana na Yehova,

  Atawafedhehesha,

  Wataangamia.

  Har–​Magedoni,

  Hawawezi kuiponyoka.

  Punde watajua

  Anaitwa Yehova.

  (KORASI)

  Yah Yehova, Uliye juu,

  Yuleyule wa tangu milele,

  Utaharibu adui zako,

  Jina lako litakaswe.