TAZAMA
Maandishi
Picha

(Luka 23:43)

 1. 1. Mungu wetu katuahidi,

  Ataleta paradiso.

  Atafuta makosa yote,

  Kisiwepo kifo kamwe.

  (KORASI)

  Paradiso, duniani.

  Twaiona, kwa imani.

  Karibuni, Kristo Yesu,

  Atafanya, yote hayo.

 2. 2. Karibuni atawaita,

  Waliomo kaburini.

  ‘Utakuwa Paradisoni,’

  Kaahidi Yesu Kristo.

  (KORASI)

  Paradiso, duniani.

  Twaiona, kwa imani.

  Karibuni, Kristo Yesu,

  Atafanya, yote hayo.

 3. 3. Sasa Kristo, anatawala.

  Paradiso, ataleta.

  Tushukuru Mungu daima,

  Sifa zake na tuimbe.

  (KORASI)

  Paradiso, duniani.

  Twaiona, kwa imani.

  Karibuni, Kristo Yesu,

  Atafanya, yote hayo.