TAZAMA
Maandishi
Picha

(2 Wakorintho 4:18)

 1. 1. Watakapoona vipofu,

  Nao viziwi wasikie,

  Watoto watakapoimba,

  Amani, shangwe ziwepo,

  Wapendwa watafufuliwa,

  Na kuishi pasipo dhambi.

  (KORASI)

  Utayaona mambo hayo,

  Ukitazama zawadi.

 2. 2. Mbwa-mwitu, mwanakondoo

  Watakula nyasi pamoja,

  Naye mvulana mdogo,

  Atawaongoza wote.

  Hakutakuwa na machozi,

  Mwisho wa maumivu, hofu.

  (KORASI)

  Utayaona mambo hayo,

  Ukitazama zawadi.