Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 WIMBO NA. 134

Watoto–Amana Kutoka kwa Mungu

Chagua Rekodi ya Sauti
Watoto–Amana Kutoka kwa Mungu
TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 127:3-5)

 1. 1. Baba apatapo mwana

  Na mama anapopata mwana,

  Amana kubwa wamepata,

  Si yao tu, peke yao.

  Ni zawadi toka kwa Mungu.

  Yeye ndiye chanzo cha uhai.

  Anawaagiza wazazi,

  Wapate kuwa na hekima.

  (KORASI)

  Mmepata amana kubwa,

  Ni urithi toka Kwake.

  Basi ninyi, wafundisheni,

  Maagizo ya Yehova.

 2. 2. Sheria zote za Mungu—

  Ziwe katika mioyo yenu.

  Wafunzeni wana na binti;

  Hiyo ndiyo kazi yenu.

  Wafundishe barabarani,

  Ulalapo na uamkapo.

  Wazikumbuke sikuzote,

  Uaminifu wadumishe.

  (KORASI)

  Mmepata amana kubwa,

  Ni urithi toka Kwake.

  Basi ninyi, wafundisheni,

  Maagizo ya Yehova.