TAZAMA
Maandishi
Picha

(Mathayo 19:5, 6)

 1. 1. Kwa staha na shangwe

  Kamba imefumwa.

  Mbele za mashahidi,

  Wameapa leo.

  (KORASI YA 1)

  Mume ameahidi,

  Kumpenda mke.

  ‘Alichounganisha,

  Kisitenganishwe.’

 2. 2. Neno lake Mungu,

  Wamelichunguza.

  Mungu awabariki;

  Watimize yote.

  (KORASI YA 2)

  Mke ameahidi,

  Kumpenda mume.

  ‘Alichounganisha,

  Kisitenganishwe.’