TAZAMA
Maandishi
Picha

(Mathayo 24:13)

 1. 1. Tunawezaje

  kuvumilia mikazo?

  Yesu katuwekea

  mfano mzuri.

  Ahadi za Mungu,

  alitafakari.

  (KORASI)

  Basi tuvumilie.

  Tulinde imani.

  Kwa kuwa Atupenda,

  Tutavumilia hadi mwisho.

 2. 2. Japo maisha

  yamejawa na uchungu;

  Twatafakari,

  Mfumo mpya wa Mungu.

  Tuwepo, tuone.

  Tumeazimia.

  (KORASI)

  Basi tuvumilie.

  Tulinde imani.

  Kwa kuwa Atupenda,

  Tutavumilia hadi mwisho.

 3.  3. Hatufi moyo

  Wala hatutaogopa.

  Tutumikie

  hadi mwisho ufikapo.

  Tuzidi kudumu,

  Mwisho u karibu.

  (KORASI)

  Basi tuvumilie.

  Tulinde imani.

  Kwa kuwa Atupenda,

  Tutavumilia hadi mwisho.