TAZAMA
Maandishi
Picha

(1 Wakorintho 16:13)

 1. 1. Uwe macho na imara,

  Azimia kudumu.

  Tenda kama mwanamume,

  Ushinde majaribu.

  Kristo Yesu msikilize,

  Usimame upande wake.

  (KORASI)

  Uwe macho na mwenye nguvu!

  Udumu hadi mwisho.

 2. 2. Uwe macho na kukesha,

  Na tayari kutii.

  Tii mwongozo wa Kristo,

  Kupitia mtumwa.

  Tii shauri la wazee,

  Walindao kondoo zake.

  (KORASI)

  Uwe macho na mwenye nguvu!

  Udumu hadi mwisho.

 3.  3. Uwe macho kutetea,

  Ukweli kwa bidii.

  Japo adui ni wengi,

  Hubiri hadi mwisho.

  Shiriki kumsifu Mungu.

  Siku Yake iko karibu.

  (KORASI)

  Uwe macho na mwenye nguvu!

  Udumu hadi mwisho.