TAZAMA
Maandishi
Picha

(Luka 17:5)

 1. 1. Kwa sababu hatujakamilika,

  Mwelekeo wetu ni mbaya.

  Kuna dhambi itutatanishayo—

  Kutokuwa na imani kwako.

  (KORASI)

  Ee, Yehova, tupatie imani.

  Twakuomba, utusaidie,

  Kwa rehema unazotuonyesha.

  Nawe uheshimiwe zaidi.

 2. 2. Ili kukupendeza wewe vema,

  Ni lazima tuwe na imani.

  Kama ngao, imani hutulinda.

  Hatuhofu tunayokabili.

  (KORASI)

  Ee, Yehova, tupatie imani.

  Twakuomba, utusaidie,

  Kwa rehema unazotuonyesha.

  Nawe uheshimiwe zaidi.