TAZAMA

(2 Petro 3:15)

 1. 1. Yehova U Mungu mkuu,

  Wapenda uadilifu.

  Nao uovu wazidi,

  Wajua twahuzunika.

  Watu wadai wakawia;

  Wakati wako utafika.

  (KORASI)

  Twatazamia kwa hamu,

  Ahadi zako zitimie.

 2. 2. Kwako miaka elfu moja,

  Ni kama siku moja tu.

  Siku yako kuu yaja.

  Kamwe haitakawia.

  Japo uovu wachukia,

  Wapenda watu wakitubu.

  (KORASI)

  Twatazamia kwa hamu,

  Ahadi zako zitimie.