Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

‘Mwimbieni Yehova kwa Shangwe’

 WIMBO NA. 111

Sababu za Kuwa na Shangwe

Chagua Rekodi ya Sauti
Sababu za Kuwa na Shangwe
TAZAMA
Maandishi
Picha

(Mathayo 5:12)

 1. 1. Tuna sababu nyingi sana,

  Kuwa na shangwe halisi.

  Watu wa mataifa yote,

  Wanajiunga na sisi.

  Tunashangilia moyoni,

  Neno linaeleweka.

  Tunajifunza kila siku;

  Imani yaongezeka.

  Nayo shangwe yetu yazidi,

  Kama moto uwakao.

  Ingawa tuna matatizo,

  Kwetu Yehova ni ngao.

  (KORASI)

  Yehova ni shangwe yetu,

  Kazi zake za ajabu.

  Mawazo yake yapita yetu,

  Mungu mwema na mkuu!

 2.  2. Tunaziona kazi zake,

  Mbingu, bahari, dunia.

  Anastahili kusifiwa,

  Kwa kazi za uumbaji.

  Sasa twatangaza ushindi,

  Wa Ufalme wa Yehova.

  Ujumbe wa baraka zake,

  Kotekote twatangaza.

  Siku mpya yakaribia,

  Sikuzote kuwe shangwe.

  Dunia nazo mbingu mpya,

  Milele tushangilie.

  (KORASI)

  Yehova ni shangwe yetu,

  Kazi zake za ajabu.

  Mawazo yake yapita yetu,

  Mungu mwema na mkuu!