TAZAMA
Maandishi
Picha

(1 Yohana 4:7, 8)

 1. 1. Mungu ni mwenye upendo,

  Hutaka tumuige.

  Upendo tukiwa nao,

  Tutatenda mema tu.

  Ndiyo siri ya maisha;

  Maisha ya Wakristo.

  Upendo kama wa Kristo,

  Kamwe hautashindwa.

 2. 2. Kupenda kweli na Mungu;

  Hutuchochea sana.

  Husamehe tukosapo;

  Nguvu anatutia.

  Upendo hauna wivu;

  Huvumilia yote.

  Na tupende ndugu zetu,

  Pasipo unafiki.

 3. 3. ’Siwe na kinyongo kamwe;

  Na kisikutawale.

  Mtegemee Yehova;

  Ufwate amri zake:

  Penda Mungu na jirani,

  Penda toka moyoni.

  Na tuonyeshe upendo

  Upendo wa Kikristo.