Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 WIMBO NA. 104

Roho Takatifu​—⁠Zawadi Kutoka kwa Mungu

Chagua Rekodi ya Sauti
Roho Takatifu​—⁠Zawadi Kutoka kwa Mungu
TAZAMA
Maandishi
Picha

(Luka 11:13)

 1. 1. Baba Yehova, mwenye rehema

  Mioyo yetu waijua.

  Tuondolee mahangaiko,

  Tupe faraja ya roho yako.

 2. 2. Twakukosea mara kwa mara.

  Tu wanadamu wenye dhambi.

  Mungu twaomba: Tunakusihi,

  Utuongoze kwa roho yako.

 3. 3. Tunapochoka, na kulemewa,

  Roho yako yatuinua.

  Tutakimbia, hatutachoka.

  Tupe roho yako takatifu.