Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

‘Mwimbieni Yehova kwa Shangwe’

 WIMBO NA. 102

“Mwasaidie Walio Dhaifu”

Chagua Rekodi ya Sauti
“Mwasaidie Walio Dhaifu”
TAZAMA
Maandishi
Picha

(Matendo 20:35)

 1. 1. Kila mmoja wetu

  Dhambi hutenda.

  Hata hivyo, Yehova

  Anatupenda.

  Ni mwenye rehema,

  Twataka kumwiga.

  Ambao ni dhaifu,

  Tusaidie.

 2. 2. Imani ya wengine,

  Imepungua.

  Kupitia maneno

  Tuwafariji.

  Walio dhaifu

  Ni wa Mungu pia.

  Tuwahangaikie,

  Waimarike.

 3. 3. Tusiwe wachambuzi,

  Tusiwakwaze.

  Tuonyeshe fadhili,

  Waimarike.

  Tuwe na bidii,

  Moyo tuwatie;

  Na tuwategemeze,

  Wafarijike.