TAZAMA
Maandishi
Picha

(Zaburi 145:12)

 1. 1. Sifu Yah, Yehova Mungu!

  Tangazeni jina lake!

  Tangaza mwisho karibu,

  Wote wasikie ujumbe.

  Yehova Mungu ameagiza

  Kwamba sasa ni wakati

  Mwanaye atawale,

  Tangaza baraka zake zijazo!

  (KORASI)

  Sifu Yah, Yehova Mungu!

  Tangazeni fahari yake!

 2. 2. Sifu Yah, na kumwimbia!

  Lisifuni jina lake!

  Kwa shangwe, toka moyoni,

  Utukufu wake tangaza.

  Mungu ni mwema kwa watu wote,

  Licha ya fahari yake.

  Anajua mahitaji yetu,

  Huitika tumwitapo.

  (KORASI)

  Sifu Yah, Yehova Mungu!

  Tangazeni fahari yake!