Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Msitu wa Biriya huko Galilaya

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, zamani nchi ya Israeli ilikuwa na misitu kama Biblia inavyosema?

BIBLIA inasema kwamba maeneo fulani ya Nchi ya Ahadi yalikuwa na misitu na miti mingi. (1 Fal. 10:27; Yos. 17:15, 18) Hata hivyo, wanapoona eneo kubwa lisilo na misitu katika Israeli ya leo, wengine wanatilia shaka ukweli wa jambo hilo.

Kishada cha tini za mikuyu

Kitabu kimoja (Life in Biblical Israel) kinaeleza kwamba “zamani kulikuwa na misitu mingi katika nchi ya Israeli kuliko ilivyo leo.” Eneo la nyanda za juu lilikuwa na misonobari (Pinus halepensis), mialoni (Quercus calliprinos), na miti ya terebinthi (Pistacia palaestina). Huko Shefela, eneo lenye milima linaloanzia kwenye safu za milima ya kati hadi Pwani ya Mediterania, kulikuwa na miti mingi ya tini za mikuyu (Ficus sycomorus).

Kitabu kingine (Plants of the Bible) kinasema kwamba maeneo fulani ya nchi ya Israeli leo hayana miti kabisa. Ni nini kimechangia jambo hilo? Kitabu hicho kinaeleza hivi kuhusu jinsi jambo hilo lilivyotokea hatua kwa hatua: “Mwanadamu ameharibu sana uoto wa asili, hasa ili kupanua mashamba na maeneo ya malisho, na vilevile kupata vifaa vya kujengea na nishati.”