Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

Kisiwa cha Ometepe kilichopo katika Ziwa la Nikaragua kimefanyizwa na milima miwili ya volkano iliyounganishwa na rasi

 NCHI NA WATU

Kutembelea Nikaragua

Kutembelea Nikaragua

MARA nyingi watu huiita Nikaragua nchi yenye maziwa na volkano. Ziwa Nikaragua ndilo ziwa kubwa zaidi katika Amerika ya Kati. Wenyeji wanaliita Cocibolca, neno linalomaanisha “Bahari Tamu.” Ziwa hilo lina mamia ya visiwa na ni ziwa pekee lenye maji baridi lililo na viumbe wa baharini kama vile papa, chuchunge, na tarpon.

Ua aina ya sacuanjoche (frangipani) ni mojawapo ya kitambulisho cha taifa la Nikaragua

Nchi ya Nikaragua ina eneo lililo mbali zaidi katika Amerika ya Kati—Pwani ya Mosquito. Pwani hiyo ina upana wa kilomita 65, ulio pembezoni mwa eneo la ufuo upande wa mashariki hadi karibu na nchi jirani ya Honduras. Wamiskito (njia ya nyingine ya kutamka jina Mosquito) ni kabila mojawapo nchini Nikaragua ambalo limekuwapo kabla hata Wazungu kuingia katika nchi hiyo katika karne ya 16.

Wamiskito hupenda kushirikiana na wana desturi za pekee. Kwa mfano, Kimiskito hakina maneno rasmi ya kutambulisha mtu kama vile “Bwana” au “Bibi.” Katika maeneo mengi ya vijijini, vijana huwaita watu waliowazidi umri, “Mjomba” au “Shangazi,” iwe ni ndugu zao  au la. Pia, ni desturi ya muda mrefu miongoni mwa Wamiskito kwa mwanamke kumsalimia rafiki wa karibu au ndugu kwa kugusana mashavu. Kisha, mwanamke aliyeanza kutoa salamu huvuta pumzi kupitia pua yake.

Wenyeji wa Nikaragua

Machapisho yanayozungumzia Biblia katika lugha ya Kimayangna na Kimiskito, yaliyochapishwa na Mashahidi wa Yehova