Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Amkeni!  |  Septemba 2015

 JE, NI KAZI YA UBUNI?

Vijidudu Vinavyomeng’enya Mafuta

Vijidudu Vinavyomeng’enya Mafuta

KATIKA mwaka wa 2010, lita milioni 800 za mafuta machafu zilimwagika katika Ghuba ya Mexico baada ya mtambo wa kuchimba mafuta kulipuka na kisha kuzama. Hata hivyo, baada ya miezi kadhaa kupita kiasi kikubwa cha uchafu huo kilitoweka. Kwa nini?

Fikiria hili: Utafiti wa kisayansi umeonyesha kwamba kundi la bakteria walio baharini wanaweza kumeng’enya kiwango kikubwa cha molekuli za kaboni kinachopatikana katika mafuta. Mwanabiolojia wa mazingira, Profesa Terry Hazen, anasema bakteria hao ni kama “makombora yanayolenga mafuta.” Bakteria hao walitumiwa pia kusafisha mafuta yaliyomwagika katika Ghuba ya Mexico kama ilivyotajwa mwanzoni.

Ripoti ya BBC ilisema hivi kuhusu jambo hilo: “Haishangazi kwamba bahari zina vijidudu vyenye uwezo wa kumeng’enya mafuta.” Kiasili, “sakafu ya bahari imekuwa ikivuja mafuta” kwa miaka mingi sana.

Ni kweli kwamba jitihada za wanadamu za kusafisha mafuta baharini zimefanikiwa. Hata hivyo, jitihada hizo za kuondoa mafuta huenda zikaleta madhara. Dawa za kemikali zinazotumiwa ili kuondoa mafuta huzuia mfumo wa asili wa kusafisha mafuta. Pia, kemikali hizo zina sumu na zinaweza kuathiri mazingira kwa muda mrefu. Hata hivyo, uwezo wa asili wa kumeng’enya mafuta wa vijidudu hivyo hufanya bahari ijisafishe bila kuleta madhara yoyote. *

Una maoni gani? Je, vijidudu vyenye uwezo wa kumeng’enya mafuta vinavyopatikana baharini vilijitokeza vyenyewe? Au vilibuniwa?

^ fu. 6 Kwa sasa haijulikani mafuta machafu yaliyomwagika katika Ghuba ya Mexico yataathiri kwa kiasi gani viumbe vinavyoishi baharini.