Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Amkeni!  |  Agosti 2015

 JE, NI KAZI YA UBUNI?

Mfumo wa Gia wa Panzi Anayeitwa Issus

Mfumo wa Gia wa Panzi Anayeitwa Issus

KWA MUDA mrefu, imedhaniwa kwamba wanadamu ndio waliogundua mfumo wa gia. Hata hivyo, mawazo hayo yamethibitishwa kuwa si ya kweli! Hivi karibuni, mfumo wa gia zinazofanya kazi kwa pamoja umegunduliwa katika mdudu mchanga anayeitwa Issus, anayepatikana katika bustani nyingi barani Ulaya. *

Panzi huyo anapokuwa mchanga anaweza kuruka kwa mwendo kasi wa mita 3.9 kwa sekunde chache tu, na kujirusha karibu mara 200 zaidi ya nguvu za uvutano! Anaweza kutoroka kwenye upeo wa macho ukipepesa jicho tu. Ili aweze kuruka, miguu miwili ya nyuma ya mdudu huyo inahitaji kutokeza msukumo uleule sahihi na kwa wakati mmoja. Ni nini siri ya usahihi huo?

Fikiria hili: Wanasayansi wamegundua mifumo miwili ya gia zinazoungana chini ya miguu ya nyuma ya kiumbe huyo. Panzi huyo anaporuka, gia hizo husaidia miguu yake miwili ifanye kazi kwa usahihi na upatano. Isingekuwa hivyo, asingeweza kuruka kwa njia nzuri!

Viumbe wakubwa wanaporuka hutegemea mfumo wa neva kupatanisha miguu yao. Lakini, kwa panzi huyo, msukumo huo wa neva ungekuwa na kasi ndogo sana. Hivyo ndio sababu mdudu huyo ana mfumo wa gia. “Kwa kawaida sisi tunafikiria gia kuwa kitu fulani tunachokiona katika mashine ambazo mwanadamu ameunda,” alisema mtunzi na mtafiti Gregory Sutton. Kisha akaongezea sababu kwa kusema hivi: “Hatukuwa tumechunguza [kila mahali] kwa ukamili.”

Una maoni gani? Je, mfumo wa gia wa panzi anayeitwa Issus ulitokana na mageuzi? Au ulibuniwa?

^ fu. 3 Gia hizo huacha kufanya kazi anapokomaa.

Pata Kujua Mengi Zaidi

VITABU NA BROSHUA

Uhai—Ulitokana na Muumba?

Ni muhimu sana kuchunguza msingi wa mambo unayoamini kuhusu chanzo cha uhai.