Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Amkeni!  |  Julai 2015

 JE, NI KAZI YA UBUNI?

Taya la Mamba

Taya la Mamba

MAMBA ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kung’ata kwa nguvu zaidi kuliko mnyama mwingine yeyote. Kwa mfano, mamba wa maji ya chumvi wanaopatikana Australia, wanaweza kung’ata kwa nguvu mara tatu zaidi ya simba au simbamarara. Pia, taya la mamba lina uwezo wa hali ya juu wa hisi. Uwezo huo unazidi ule wa ncha ya kidole cha mwanadamu. Hilo linawezekanaje ukizingatia kwamba ngozi ya mamba ina magamba?

Taya la mamba limefunikwa kwa maelfu ya viungo vya hisi. Baada ya kufanya uchunguzi, mtafiti Duncan Leitch aliandika hivi: “Kila neva imeunganishwa na fuvu la kichwa.” Mpangilio huo unalinda nyuzi za neva zilizo katika taya na kufanya sehemu fulani za taya ziwe na uwezo mkubwa wa kuhisi. Kwa sababu ya kuwa na uwezo huo, mamba anaweza kutofautisha mdomoni mwake kati ya chakula na uchafu. Hilo pia linamwezesha mamba jike kubeba watoto wake kwa kutumia mdomo bila kuwaua. Taya la mamba lina uwezo mkubwa wa kung’ata kwa nguvu na uwezo mkubwa wa hisi.

Una maoni gani? Je, taya la mamba lilijitokeza lenyewe? Au lilibuniwa?

Pata Kujua Mengi Zaidi

VITABU NA BROSHUA

Uhai—Ulitokana na Muumba?

Ni muhimu sana kuchunguza msingi wa mambo unayoamini kuhusu chanzo cha uhai.

VIJANA HUULIZA

Uumbaji au Mageuzi?—Sehemu ya 2: Kwa Nini Uchunguze Nadharia ya Mageuzi?

Mambo matatu ya msingi yanaonyesha kwa nini unapaswa kufanya hivyo.