Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Amkeni!  |  Mei 2015

 JE, NI KAZI YA UBUNI?

Kiungo cha Ngisi wa Hawaii Kinachotoa Mwangaza

Kiungo cha Ngisi wa Hawaii Kinachotoa Mwangaza

AKIWA mwindaji wa usiku, ngisi wa Hawaii hutokeza mwangaza ili asionekane na afanane na mwangaza wa mwezi na nyota. Bakteria wanaotoa mwangaza humsaidia mnyama huyo kufanya hivyo. Ushirikiano huo unaweza kufunua siri ambazo zinaweza kutunufaisha katika njia tusiyotarajia. Inaweza kuboresha afya yetu.

Fikiria hili: Ngisi wa Hawaii huishi katika eneo lenye maji safi kwenye fuo za visiwa vya Hawaii. Kwa kawaida, mwangaza wa mwezi na nyota ungefanya vivuli vya wanyama hao vionekane na wanyama wawindaji walio chini yao. Hata hivyo, ngisi hutokeza mwangaza katika mwili wake unaofanana na mwangaza wa usiku kwa ukubwa na umbali. Jambo hilo husababisha umbo na kivuli cha mnyama huyo kisionekane. Kiungo “tata” cha ngisi kinachotoa mwangaza kina bakteria wanaotoa mwangaza unaotosha kumwezesha asionekane na wanyama wawindaji.

Bakteria hao wanaweza pia kumsaidia ngisi kudumisha utaratibu wa kulala na kuamka. Jambo hili linawavutia watafiti kwa sababu huenda ngisi si kiumbe pekee anayetegemea bakteria ili kudumisha mzunguko wa siku au utaratibu wa kulala na kuamka. Kwa mfano, katika wanyama, bakteria wanaosaidia umeng’enyaji huhusika pia katika kudumisha utaratibu wa kibiolojia wa saa 24. Kuvurugwa kwa utaratibu huo kumehusianishwa na kushuka moyo, ugonjwa wa kisukari, unene kupita kiasi, na kukosa usingizi. Hivyo, kujifunza kuhusu bakteria walio katika mwili wa ngisi kunaweza kuongeza ujuzi kuhusu afya ya mwanadamu.

Una maoni gani? Je, kiungo cha ngisi wa Hawaii kinachotoa mwangaza kimejitokeza chenyewe? Au kilibuniwa?

Pata Kujua Mengi Zaidi

VITABU NA BROSHUA

Uhai—Ulitokana na Muumba?

Ni muhimu sana kuchunguza msingi wa mambo unayoamini kuhusu chanzo cha uhai.