Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 JE, NI KAZI YA UBUNI?

Uwezo wa Ajabu wa Kusikia wa Nondo Anayeitwa Greater Wax Moth

Uwezo wa Ajabu wa Kusikia wa Nondo Anayeitwa Greater Wax Moth

NONDO anayeitwa greater wax moth ana uwezo mkubwa wa kusikia kuliko kiumbe chochote duniani. Hata hivyo, masikio yake yameumbwa kwa njia isiyo tata huku kila sikio lake likiwa na ukubwa sawa na kichwa cha pini ndogo.

Fikiria hili: Kwa miaka mingi uwezo wa nondo wa kusikia umekuwa ukifanyiwa utafiti. Hivi karibuni, wanasayansi katika chuo cha Strathclyde, Scotland, wamepima uwezo wa nondo wa kusikia kwa kutumia viwango mbalimbali vya sauti. Wamepima mitetemo ya viwambo katika sikio na kurekodi utendaji wa neva za kusikia. Viwambo vya masikio vilitetema mara 300 baada ya kupokea sauti kulingana na kipimo cha kilohati. Kwa kulinganisha, mwangwi wa popo umerekodiwa kufikia kilohati 212, uwezo wa kusikia wa pomboo ni kilohati 160, na binadamu hauzidi kilohati 20.

Watafiti wangependa kutumia uwezo huo mkubwa wa nondo kuanzisha teknolojia mpya. Jinsi gani? Daktari wa chuo kikuu cha Strathclyde, James Windmill anasema hivi: “Hii itasaidia kutengeneza vikuza-sauti vidogo vyenye ubora vinavyoweza kutumiwa katika simu za mkononi na vifaa vya kuwasaidia watu kusikia.”

Una maoni gani? Je, uwezo wa kusikia wa nondo anayeitwa great wax moth ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?