Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 HABARI KUU

Uhai Ulianzaje?

Uhai Ulianzaje?

Ungejibuje?

UHAI ULITOKANA NA ․․․․․.

  1. MAGEUZI

  2. UUMBAJI

HUENDA watu wanaopenda sayansi wakachagua “mageuzi,” na wanaopenda dini wakachagua “uumbaji.”

Lakini, majibu hayawi hivyo siku zote.

Rama Singh, profesa katika Chuo Kikuu cha McMaster nchini Kanada anasema: “Nadharia ya mageuzi imepingwa si na wanadini peke yao bali pia na watu wengi wenye elimu.”

Kwa mfano, Gerard, profesa wa elimu ya wadudu alifundishwa nadharia ya mageuzi shuleni. Anasema hivi: “Nilipofanya mitihani niliandika majibu ambayo maprofesa walitaka lakini sikuamini mambo hayo.”

Kwa nini baadhi ya wanasayansi hawakubali kuwa uhai ulitokana na mageuzi? Ili kujibu swali hilo, acheni tuchunguze maswali mawili yanayowatatanisha watafiti wengi: (1) Uhai ulianzaje? na (2) Viumbe vilitoka wapi?