Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Amkeni!  |  Oktoba 2014

 HABARI KUU | MAFANIKIO YA KWELI YANAPATIKANA JINSI GANI?

Wewe Hupimaje Mafanikio?

Wewe Hupimaje Mafanikio?

Ili ujipime, fikiria hali zifuatazo.

Ni yupi ambaye ungesema amefanikiwa kikweli?

 • ALEX

  Alex ni mfanyabiashara. Yeye ni mnyoofu, anafanya kazi kwa bidii, na ni mwenye adabu. Biashara ya Alex imesitawi, na hivyo yeye na familia yake wanaishi vizuri.

 • CAL

  Cal pia anafanya biashara kama ya Alex, lakini ana pesa nyingi zaidi. Ili afanikiwe, Cal hufanya kazi kupita kiasi na amepatwa na magonjwa mbalimbali.

 • JANET

  Janet ni mwanafunzi mwenye bidii na anapenda masomo. Kwa sababu ya bidii yake, yeye hupata alama nzuri.

 • ELLEN

  Ellen hupata alama za juu kuliko Janet na ni mwanafunzi anayeheshimiwa—lakini yeye huiba mitihani na hapendi masomo.

Ikiwa umesema Cal na Ellen—au wote wanne—wamefanikiwa, huenda unapima mafanikio kwa kuangalia tu matokeo, bila kujali jinsi matokeo hayo yalivyopatikana.

Kwa upande mwingine, ikiwa umechagua Alex na Janet, huenda umepima mafanikio kwa kuangalia sifa za mtu na maadili ya kazi. Inafaa kufanya hivyo. Fikiria mifano ifuatayo.

 • Ni jambo gani litakalomletea Janet faida za kudumu—je, ni kupata alama za juu au ni kupenda masomo?

 • Watoto wa Alex wanahitaji nini? Je, wanahitaji kununuliwa chochote wanachotaka, au wanahitaji baba anayewapenda na anayetumia muda pamoja nao?

Jambo kuu: Mafanikio ya uwongo yanategemea mambo yanayoonekana; mafanikio ya kweli hutegemea maadili yanayofaa.