Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Amkeni!  |  Julai 2014

 NCHI NA WATU | IRELAND

Kutembelea Ireland

Kutembelea Ireland

KISIWA hicho kinachoitwa pia “Emerald Isle” (Kisiwa cha Kijani) kina nchi mbili: nchi kubwa ni Jamhuri ya Ireland, na nchi ndogo ni Ireland Kaskazini, ambayo ni sehemu ya Uingereza.

Giant’s Causeway

Kisiwa cha Ireland kinaitwa Kisiwa cha Kijani kwa sababu kina mvua nyingi inayofanya sehemu kubwa ya nchi hiyo kuwa kijani. Mito na maziwa maridadi kutia ndani miinuko ya pwani pamoja na vilima huchangia uzuri wa nchi hiyo.

Nyumba iliyoezekwa kwa nyasi

Wakaaji wa Ireland wamekabili shida nyingi. Kwa mfano, inakadiriwa kwamba kati ya mwaka 1845 hadi 1851, karibu watu milioni moja walikufa kwa njaa na magonjwa mimea ya viazi ilipoharibiwa na ugonjwa. Ili kukimbia umaskini mkubwa watu wengi walihamia nchi nyingine kama vile Australia, Kanada, Marekani, na Uingereza. Leo, karibu Wamarekani milioni 35 wana asili ya Ireland.

Wenyeji wa Ireland wanajulikana kuwa wachangamfu na wakarimu. Wanapenda sana mbio za farasi, michezo kama vile kriketi, raga, mpira wa miguu, na mchezo wa Gaelic (unaofanana na mpira wa miguu). Wanawake wanapenda mchezo uitwao camogie, unaofanana na mpira wa magongo.

Bendi ya wenyeji wa Ireland

 Watu wa Ireland hupenda pia mazungumzo na muziki. Dansi ya Ireland (step dance) ni maarufu duniani kote. Wachezaji hukaza sehemu ya juu ya mwili na kuchezesha miguu yao kwa ustadi mkubwa.

Mashahidi wa Yehova wamekuwa nchini Ireland kwa zaidi ya miaka mia moja. Sasa, zaidi ya Mashahidi 6,000 huko Ireland wanawafundisha watu Biblia.

Muziki wa asili wa Ireland huchezwa kwa ala zilizo hapa chini, kuanzia kushoto kwenda kulia: kinubi cha Kiselti, zumari iitwayo bagpipe, fidla, kodiani, filimbi, na ngoma iitwayo bodhran

JE, WAJUA?

Eneo la Giant’s Causeway lililo kwenye pwani ya kaskazini ya Ireland Kaskazini, lina maelfu ya nguzo za mawe zilizotokana na lava iliyotiririka na kuingia baharini.