Kuanzia toleo hili, Amkeni! litakuwa na alama za kukusaidia upate haraka habari kutoka kwenye tovuti yetu (QR codes). Unahitaji tu kuwa na kompyuta ndogo (tablet) iliyo na kamera na iliyounganishwa kwenye Intaneti au simu aina ya smartphone.

  1.   Pakua programu inayoweza kusoma alama za QR.
  2.   Fungua programu hiyo.
  3.   Pitisha kamera juu ya alama hizo za QR.

Utaelekezwa moja kwa moja kwenye Tovuti yetu!