KATI ya ndege wote wahamaji, safari ya chamchanga anayeitwa bar-tailed ndiyo safari yenye kustaajabisha zaidi. Ndege huyo anaweza kusafiri kwa zaidi ya siku nane akienda umbali wa kilomita 11,000.

Fikiria hili: Watafiti fulani wanaamini kwamba aina fulani za ndege hutumia nguvu za sumaku za dunia ili kuwaongoza wanaposafiri, kana kwamba wana dira ndani ya ubongo wao. Zaidi ya hilo, inawezekana kwamba chamchanga huyo hutumia jua kumwongoza wakati wa mchana na nyota wakati wa usiku. Pia inaonekana kwamba chamchanga huyo anaweza kutambua ikiwa kuna dhoruba inayokuja na hivyo atumie upepo wake ili umsukume. Hata hivyo, bado wataalamu hawajui mambo yote yanayomwezesha ndege huyo kusafiri kwa njia hiyo yenye kustaajabisha. Mwanabiolojia Bob Gill anasema, “Nimekuwa nikiwachunguza kwa miaka 20 na bado safari yao huniacha kinywa wazi.”

Una Maoni Gani? Je, mfumo wa kumwongoza chamchanga anayeitwa bar-tailed ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?