Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Amkeni!  |  Oktoba 2012

Kuutazama Ulimwengu

Kuutazama Ulimwengu

“Karibu nusu ya watu wanaogunduliwa kuwa na ugonjwa wa kansa nchini Uingereza kila mwaka, yaani, zaidi ya watu 130,000, wanaupata kwa sababu ya kufanya mambo ambayo wangeweza kuepuka kama vile kuvuta sigara, kunywa kupindukia na kula vyakula visivyo na lishe.”—SHIRIKA LA HABARI LA BBC, UINGEREZA.

“Biashara kubwa ya magendo ya kuuza viungo vya wanyama-pori inaangamiza wanyama wanaopendwa sana ulimwenguni . . . kwa kiwango kikubwa sana kuliko wakati mwingine wowote.”—SHIRIKA LA KUHIFADHI WANYAMA-PORI, MAREKANI.

Watu ambao kwa wastani hutazama televisheni kwa saa sita kila siku wanaweza kutazamia kwamba umri wao utapungua kwa miaka 4.8 kuliko wale ambao hawatazami televisheni. Kwa maneno mengine, kila saa moja ambayo mtu mzima hutumia kutazama televisheni hupunguza uhai wake kwa dakika 22 hivi.BRITISH JOURNAL OF SPORTS MEDICINE, UINGEREZA.

Nchini Ujerumani, zaidi ya asilimia 90 ya wanawake ambao watoto wao walio tumboni wanagunduliwa kuwa wana tatizo la Down syndrome huamua kutoa mimba hiyo.DER TAGESSPIEGEL, UJERUMANI.

Mfadhaiko Unaotokana na Maisha ya Mjini

Utafiti umeonyesha kwamba “watu wanaoishi kwenye majiji hutenda kwa jeuri wanapofadhaika kuliko wale wanaoishi kwenye miji midogo,” linasema gazeti Przekrój la Poland. “Majiji yana vitu vingi ambavyo vinaweza kuchochea mfadhaiko,” anasema mwanasaikolojia Mieczysław Jaskulski katika Kituo cha Elimu na Utafiti Kuhusu Matatizo ya Akili cha Warsaw. “Kwa watu wanaoishi katika majiji, uwezekano wa kuwa na tatizo la kushikwa na wasiwasi kwa ghafula ni asilimia 21 zaidi ya wale wanaoishi katika maeneo ya vijijini, na uwezekano wa kupatwa na tatizo la kubadilika-badilika kwa hisia ni asilimia 39 zaidi kwa wale wanaoishi jijini.” Watu wanaoishi kwenye majiji wanaweza kukabilianaje na hatari hiyo? “Usikatishwe tamaa na mambo ambayo huwezi kuyadhibiti,” “usiendelee kufikiria kazi baada ya kuondoka kazini,” “nenda matembezi,” na “usiogope kuchukua likizo,” linapendekeza gazeti Przekrój.

Kituo cha Facebook Kinahifadhi Habari Nyingi Kiasi Gani?

Mwanafunzi anayesomea mambo ya sheria nchini Austria alitaka kujua ni kiasi gani cha habari kumhusu kilichokuwa kimehifadhiwa na kituo kikubwa zaidi cha mawasiliano ulimwenguni katika kipindi cha miaka mitatu ambayo alikuwa amejiandikisha katika kituo hicho, kwa hiyo akaomba atumiwe nakala ya habari hizo. Kituo cha Facebook kilimtumia mwanafunzi huyo CD iliyokuwa na kurasa 1,222 zilizokuwa na habari zake. Kama ilivyotaarifiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Der Tagesspiegel, mwanafunzi huyo alisema hivi: “Habari zote zilikuwa zimehifadhiwa kutia ndani, kila ujumbe, mazungumzo yote, na hata habari za siri kuhusu rafiki zangu.” Alitumiwa pia ujumbe wote ambao alikuwa na uhakika kuwa amefuta!