Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 HABARI KUU | KUSHINDA KIZUIZI CHA LUGHA

Kushinda Kizuizi cha Tangu Zamani

Kushinda Kizuizi cha Tangu Zamani

LEO kuna lugha nyingi tofauti-tofauti duniani, karibu lugha 7,000 hivi. Hilo hutokeza changamoto katika nyanja ya usafiri, biashara, na serikali. Hali imekuwa hivyo tangu zamani. Kwa mfano, miaka 2,500 hivi iliyopita, katika utawala wa Mfalme Ahasuero (huenda ni Shasta wa I), Waajemi walituma ujumbe katika milki yote, “kutoka India mpaka Ethiopia, wilaya za utawala 127, kila wilaya ya utawala kwa mtindo wao wa kuandika na kila kikundi cha watu kwa lugha yao.” *

Leo, mashirika au hata serikali nyingi zimeshindwa kufanya jambo gumu kama hilo. Lakini kuna shirika moja ambalo limefaulu kufanya kazi hiyo kwa ustadi. Mashahidi wa Yehova huchapisha magazeti, rekodi za kusikiliza, video, na vitabu vingi kutia ndani Biblia katika lugha zaidi ya 750. Hilo linatia ndani lugha za ishara [alama] 80. Pia, Mashahidi wanatafsiri machapisho mbalimbali katika Maandishi ya vipofu.

Zaidi ya yote, Mashahidi wa Yehova hawapati faida ya kiuchumi kwa sababu ya jitihada zao. Kwa kweli, watafsiri na wafanyakazi wengine hufanya kazi kwa kujitolea. Kwa nini wanafanya kazi ngumu ya kutafsiri lugha nyingi, nao hufanya kazi hiyo jinsi gani?

^ fu. 3 Soma Esta 8:9 katika Biblia.