Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo  |  Oktoba 2016

 HAZINA ZA NENO LA MUNGU | METHALI 12-16

Hekima Ni Bora Kuliko Dhahabu

Hekima Ni Bora Kuliko Dhahabu
TAZAMA
Maandishi
Picha

Kwa nini hekima kutoka kwa Mungu ina thamani kubwa? Kwa sababu inawakomboa wenye hekima kutokana na njia mbaya na kuwahifadhi hai. Inamsaidia mtu kuwa na mtazamo, maneno, na matendo mazuri.

Hekima inatulinda tusiwe na kiburi

16:18, 19

  • Mtu mwenye hekima anatambua kwamba Yehova ni Chanzo cha hekima yote

  • Wale waliofanikiwa au walio na mapendeleo wanapaswa kujilinda wasiwe na kiburi na majivuno

Hekima humsaidia mtu kusema maneno yanayofaa

16:21-24

  • Mtu mwenye hekima anatumia utambuzi kufahamu mambo mazuri ya wengine na huzungumza vizuri kuwahusu

  • Maneno yenye hekima yana manufaa na ni matamu kama asali, si maneno makali au ya uchokozi