Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha  |  Machi 2017

 HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YEREMIA 12-16

Waisraeli Walimsahau Yehova

Waisraeli Walimsahau Yehova

Yeremia alipewa mgawo mgumu ambao ungeonyesha jinsi Yehova alivyoazimia kuangamiza Yuda na Yerusalemu yenye kiburi.

Yeremia alinunua mshipi wa kitani

13:1, 2

  • Mshipi uliofungwa kiunoni uliwakilisha uhusiano wa karibu kati ya Yehova na taifa hilo

Yeremia aliupeleka mshipi huo kwenye Mto Efrati

13:3-5

  • Aliuficha kwenye mpasuko wa mwamba kisha akarudi Yerusalemu

Yeremia alirudi kwenye Mto Efrati kuuchukua mshipi

13:6, 7

  • Mshipi ulikuwa umeharibika

Baada ya Yeremia kutekeleza mgawo wake ndipo Yehova alimweleza kilichomaanishwa na mfano huo

13:8-11

  • Utii wa Yeremia wa kutoka moyoni katika jambo ambalo lilionekana kuwa dogo ulitimiza fungu muhimu katika jitihada za Yehova za kufikia mioyo ya watu wake