Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Chagua lugha Kiswahili

 HAZINA ZA NENO LA MUNGU | ESTA 6-10

Esta Alimtanguliza Yehova na Watu Wake

Esta Alimtanguliza Yehova na Watu Wake
TAZAMA
Maandishi
Picha

Esta alikuwa jasiri na aliwatanguliza wengine alipomtetea Yehova na watu wake

8:3-5, 9

  • Esta na Mordekai walikuwa salama. Lakini agizo la Hamani la kuwaua Wayahudi lilikuwa likisambazwa kotekote katika milki ya Ahasuero

  • Esta alihatarisha uhai wake tena kwa kwenda mbele ya mfalme bila kuitwa. Alilia kwa ajili ya watu wake na kumwomba mfalme afutilie mbali agizo alilokuwa ametoa

  • Sheria zilizopitishwa katika jina la mfalme hazingebadilishwa. Hivyo, mfalme alimpa Esta na Mordekai mamlaka ya kuandika sheria mpya

Yehova aliwapa watu wake ushindi mkubwa

8:10-14, 17

  • Tangazo la pili lilitolewa la kuwapa Wayahudi haki ya kujilinda

  • Wapanda-farasi wakaenda upesi kila sehemu ya milki hiyo na Wayahudi wakajitayarisha kupigana

  • Watu wengi waligeuzwa imani na kuwa wafuasi wa dini ya Wayahudi kwa sababu waliona uthibitisho kwamba Wayahudi wana kibali cha Mungu