Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha  |  Januari 2018

 HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MATHAYO 8-9

Yesu Aliwapenda Watu

Yesu Aliwapenda Watu

Mathayo sura ya 8 na 9 zinaonyesha sehemu fulani ya huduma ya Yesu katika eneo la Galilaya. Yesu alipowaponya watu, alionyesha nguvu zake, lakini jambo muhimu hata zaidi ni kwamba alionyesha upendo na huruma kwa ajili ya wengine.

 1. Yesu alimponya mtu mwenye ukoma.—Mt 8:1-3

 2. Yesu alimponya mtumishi wa ofisa wa jeshi.—Mt 8:5-13

  Alimponya mama mkwe wa Petro.—Mt 8:14, 15

  Aliwafukuza roho waovu na kuponya watu waliokuwa wakiteseka.—Mt 8:16, 17

 3. Yesu alifukuza roho waovu wakali sana, na wakaingia ndani ya kundi la nguruwe.—Mt 8:28-32

 4. Yesu alimponya mtu aliyepooza.—Mt 9:1-8

  Alimponya mwanamke aliyegusa vazi lake, na akamfufua binti ya Yairo.—Mt 9:18-26

  Aliponya vipofu na mabubu.—Mt 9:27-34

 5. Yesu alitembelea majiji na vijiji, akiponya kila aina ya ugonjwa na kila aina ya udhaifu.—Mt 9:35, 36

Ninaweza kuwaonyeshaje upendo na huruma zaidi wale wanaonizunguka?