Mfalme Senakeribu wa Ashuru alimtuma Rabshake Yerusalemu akawaambie watu wa jiji hilo wasalimu amri. Waashuru walitoa hoja mbalimbali za kuwafanya Wayahudi wasalimu amri bila kupigana.

  • Hakuna atakayewasaidia. Misri haitawasaidia.—Isa 36:6

  • Shaka. Yehova hatawapigania kwa sababu mmemuudhi.—Isa 36:7, 10

  • Vitisho. Hamwezi kulishinda jeshi lenye nguvu la Waashuru.—Isa 36:8, 9

  • Vishawishi. Kujisalimisha kwa Waashuru kutaboresha maisha yenu.—Isa 36:16, 17

Hezekia alikuwa na imani thabiti katika Yehova

37:1, 2, 14-20, 36

  • Alifanya yote awezayo kutayarisha jiji kwa ajili ya kuzingirwa

  • Alimwomba Yehova awakomboe na aliwatia moyo watu wafanye hivyo pia

  • Imani yake ilithawabishwa Yehova alipomtuma malaika na kuwaua mashujaa 185,000 wa Ashuru katika usiku mmoja