Vipimo vya ufikikaji

Chagua lugha

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Hamia kwenye habari

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

DAFTARI LA MKUTANO WA HUDUMA NA MAISHA YETU YA KIKRISTO DESEMBA 2016

 HAZINA ZA NENO LA MUNGU | ISAYA 17-23

Kutumia Mamlaka Vibaya Humfanya Mtu Apoteze Mapendeleo

Kutumia Mamlaka Vibaya Humfanya Mtu Apoteze Mapendeleo

Shebna alikuwa msimamizi-nyumba. Huenda alisimamia nyumba ya Mfalme Hezekia. Alikuwa wa pili kutoka kwa Mfalme na alitarajiwa atimize mengi.

22:15, 16

  • Shebna alipaswa kuhangaikia mahitaji ya watu wa Mungu

  • Kwa ubinafsi alijitafutia utukufu

22:20-22

  • Yehova alimnyang’anya Shebna mamlaka na kumpa Eliakimu

  • Eliakimu alikabidhiwa “ufunguo wa nyumba ya Daudi,” unaowakilisha nguvu na mamlaka

Fikiria hili: Shebna alipaswa kutumiaje mamlaka yake kuwasaidia wengine?