Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Biblia Kwenye Mtandao | BIBLIA TAKATIFU—TAFSIRI YA ULIMWENGU MPYA (TOLEO LA 2017)

Esta 6:1-14

MUHTASARI WA YALIYOMO

  • Mordekai aheshimiwa na mfalme (1-14) (1-14)

6  Usiku huo mfalme hakupata usingizi.* Hivyo, akaagiza kitabu cha historia ya nyakati kiletwe,+ nacho kikasomwa mbele yake.  Wakapata kwamba kilikuwa kimeandikwa habari ambazo Mordekai alitoa kuhusu Bigthana na Tereshi, wale maofisa wawili wa makao ya mfalme, walinzi wa milango, waliopanga njama ya kumuua Mfalme Ahasuero.+  Mfalme akauliza: “Mordekai amepewa heshima na shukrani gani kwa tendo hilo?” Ndipo watumishi binafsi wa mfalme wakasema: “Hajafanyiwa jambo lolote.”  Baadaye mfalme akauliza: “Ni nani aliye katika ua?” Basi Hamani alikuwa amekuja katika ua wa nje+ wa nyumba ya* mfalme ili azungumze na mfalme kuhusu kumtundika Mordekai juu ya mti aliokuwa ameutengeneza kwa ajili yake.+  Watumishi wa mfalme wakamjibu: “Ni Hamani+ aliyesimama kwenye ua.” Mfalme akasema: “Mwambieni aingie.”  Hamani alipoingia, mfalme akamwambia: “Afanyiwe nini mtu ambaye mfalme angependa kumheshimu?” Hamani akajiambia moyoni: “Mfalme angependa kumheshimu nani isipokuwa mimi?”+  Basi Hamani akamwambia mfalme: “Mtu ambaye mfalme angependa kumheshimu,  na aletewe mavazi ya kifalme+ ambayo mfalme huvaa na farasi ambaye humbeba mfalme, farasi mwenye taji la kifalme kichwani.  Kisha mmoja wa wakuu wa cheo cha juu wa mfalme apewe hayo mavazi na yule farasi, nao wanapaswa kumvisha mtu ambaye mfalme angependa kumheshimu, na wamtembeze katika uwanja wa jiji akiwa juu ya farasi. Kisha wanapaswa kutangaza kwa sauti mbele yake: ‘Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme angependa kumheshimu!’”+ 10  Mara moja mfalme akamwambia Hamani: “Fanya haraka! Chukua mavazi na farasi, nawe umfanyie Mordekai kama ulivyosema, yule Myahudi anayeketi katika lango la mfalme. Usikose kumfanyia lolote kati ya mambo uliyosema.” 11  Basi Hamani akachukua mavazi hayo na farasi, akamvisha Mordekai+ na kumtembeza katika uwanja wa jiji akiwa juu ya farasi na kutangaza kwa sauti mbele yake: “Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme angependa kumheshimu!” 12  Baadaye Mordekai akarudi kwenye lango la mfalme, lakini Hamani akaenda haraka nyumbani kwake, akiomboleza akiwa amefunika kichwa chake. 13  Hamani alipomsimulia Zereshi mke wake+ na marafiki zake wote mambo yaliyompata, watu wake wenye hekima na Zereshi mke wake wakamwambia: “Ikiwa Mordekai ambaye umeanza kuanguka mbele yake ni wa uzao wa Kiyahudi,* hutaweza kumshinda; kwa hakika utaanguka mbele yake.” 14  Walipokuwa wakizungumza naye, maofisa wa makao ya mfalme wakaja na kumchukua Hamani na kumpeleka haraka kwenye karamu ambayo Esta alikuwa ameandaa.+

Maelezo ya Chini

Tnn., “usingizi wa mfalme ulitoweka.”
Au “jumba la.”
Tnn., “anatokana na mbegu ya Wayahudi.”