Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Hamia kwenye yaliyomo

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

Biblia Kwenye Mtandao | BIBLIA TAKATIFU—TAFSIRI YA ULIMWENGU MPYA (TOLEO LA 2017)

Ayubu 18:1-21

MUHTASARI WA YALIYOMO

  • Bildadi azungumza kwa mara ya pili (1-21)

    • Aeleza yatakayowapata waovu (5-20)

    • Adai Ayubu hamjui Mungu (21)

18  Bildadi+ Mshua akajibu:   “Utaendelea kusema maneno haya mpaka lini? Onyesha uelewaji kidogo ili nasi tuseme.   Kwa nini tuonwe kama wanyama+Na kuonekana wapumbavu* machoni pako?   Hata ukijirarua* vipandevipande kwa hasira,Je, dunia itaachwa kwa ajili yako,Au mwamba kuhama mahali pake?   Naam, nuru ya mwovu itazimwa,Na mwali wa moto wake hautang’aa.+   Hakika nuru iliyo ndani ya hema lake itakuwa giza,Na taa iliyo juu yake itazimwa.   Hatua zenye nguvu zimefupishwa,Na shauri lake mwenyewe litamwangusha.+   Kwa maana miguu yake itamwongoza kwenye wavu,Naye atatangatanga kwenye kamba za wavu.   Mtego utamnasa kisigino;Na kitanzi kitamkamata.+ 10  Kamba imefichwa ardhini kwa ajili yake,Na mtego uko kwenye kijia chake. 11  Vitisho vinamwogopesha pande zote+Na kumfuatia miguuni pake. 12  Nguvu zake zimepungua,Na msiba+ utamfanya ayumbeyumbe.* 13  Ngozi yake imeliwa;Ugonjwa hatari sana unakula* viungo vyake. 14  Ameng’olewa kutoka katika hema lake lililo salama+Na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.* 15  Wageni watakaa* katika hema lake;Kiberiti kitatawanywa juu ya makao yake.+ 16  Chini yake, mizizi yake itakauka,Na juu yake, matawi yake yatanyauka. 17  Hakuna atakayemkumbuka duniani,Na jina lake halitajulikana* mtaani. 18  Ataondolewa kwenye nuru na kupelekwa gizaniNa kufukuzwa kutoka duniani.* 19  Hatakuwa na mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake,Wala hakuna atakayebaki katika makao yake.* 20  Siku yake itakapofika, watu wa Magharibi watashtuka sanaNa watu wa Mashariki watashikwa na hofu. 21  Hivyo ndivyo inavyokuwa kwa mahema ya mkosajiNa kwa makao ya mtu ambaye hajamjua Mungu.”

Maelezo ya Chini

Au labda, “wasio safi.”
Au “ukiirarua nafsi yako.”
Au “achechemee.”
Tnn., “Mzaliwa wa kwanza wa kifo anakula.”
Au “kifo kinachotisha.”
Tnn., “Kitu ambacho si chake kitakaa.”
Tnn., “hatakuwa na jina.”
Au “kwenye ardhi inayozaa.”
Au “makao yake ya muda.”